Kenya: Azimio waweka mikakati ya kumvumisha Raila magharibi

Kenya: Azimio waweka mikakati ya kumvumisha Raila magharibi

VIONGOZI wa Azimio la Umoja, One Kenya kutoka Magharibi mwa Kenya, wanatarajiwa kumfanyia kampeni mgombeaji urais wa muungano huo Raila Odinga, baada ya kukamilishwa kwa kura za mchujo.

Kampeni hizo zitaendeshwa na afisi kuu ya muungano inayoongozwa na Mshirikishi wa Kampeni za Urais za Bw Odinga katika Ukanda wa Nyanza, Gavana wa Siaya Cornel Rasanga.

Magavana kutoka eneo pana la Magharibi mwa Kenya, Jumanne walikutana katika makao makuu ya Azimio, Kisumu, kujadili mipango ya kampeni za muungano huo.

“Afisi kuu imejiandaa ili baada ya vyama tanzu kukamilisha kura za mchujo tutaanza rasmi kampeni ya kumvumisha Bw Odinga,” akasema Bw Rasanga.

Asante kwa kushiriki!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *