Brighton yadidimiza matumaini ya Arsenal kumaliza msimu wa EPL ndani ya 4-bora jedwalini

Brighton yadidimiza matumaini ya Arsenal kumaliza msimu wa EPL ndani ya 4-bora jedwalini

ARSENAL walididimiza matumaini yao ya kukamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu ndani ya orodha ya nne-bora na hivyo kufuzu kwa soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) msimu ujao baada ya Brighton kuwatandika 2-1 mnamo Jumamosi ugani Emirates.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Brighton kushinda mechi baada ya michuano saba iliyopita. Walifungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Leandro Trossard kabla ya Enock Mwepu kupachika wavuni goli la pili.

Arsenal ya kocha Mikel Arteta ilirejeshwa mchezoni mwishoni mwa kipindi cha pili kupitia bao la Martin Odegaard. Kikosi hicho sasa kinakamata nafasi ya tano kwa alama 54, tatu zaidi nyuma ya Tottenham Hotspur waliotandika Aston Villa 4-0.

Brighton walipaa hadi nafasi ya 11 kwa pointi 37 sawa na Leicester City na Crystal Palace licha ya kushinda mechi ya nne pekee kati ya 26 zilizopita katika EPL.

MATOKEO YA EPL (Jumamosi):

Everton 1-0 Man-United

Arsenal 1-2 Brighton

Southampton 0-6 Chelsea

Watford 0-3 Leeds

Aston Villa 0-4 Tottenham

Asante kwa kushiriki!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *