Kenya:Otuoma anyakua tikiti ya ODM kwa ugavana Busia

Kenya:Otuoma anyakua tikiti ya ODM kwa ugavana Busia

ALIYEKUWA mbunge wa Funyula, Dkt Paul Otuoma atapeperusha bendera ya ODM kuwania kiti cha ugavana Busia, baada ya kumshinda Mbunge Mwakilishi wa Kike, Bi Florence Mutua kwenye kura za mchujo za chama hicho.

Otuoma alipata kura 49,330 dhidi ya 30,996 za Bi Mutua.Matokeo ya mchujo huo yalitangazwa na Prof Charles Tipps katika Chuo cha kutoa mafunzo ya Kilimo (ATC) mjini Busia.

Akihutubia wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi Otuoma alikiri shughuli hiyo ilitendeka kwa usawa na uwazi,huku akiahihidi kushirikiana na wote waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali kwenye chama hicho kuelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Source: Taifaleo

Asante kwa kushiriki!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *